Baadhi ya vipodozi vya aina mbalimbali vikiwa katika moja ya maduka mkoani Iringa tayari kwa watumiaji kuja kuvinunua. (Picha na Sabinus Paulo) |
John Masanja,
Mwandishi Iringa Kwetu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Nyanda za Juu Kusini imetoa tahadhali kwa watu wanaoendelea kutumiwa vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani ni hatari kwa faya zao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mamlaka ili kudhibiti bidhaa hizo.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa gazeti la Iringa Kwetu Mkaguzi wa Dawa, TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dk Sylvester Mwidunda amesema kuwa mamlaka hiyo imebaini kuwa bado suala la utengenezaji, usambazaji na uuzaji wa vipodozi
vyenye sumu unaendelea.
Mwidunda amesema “Kwa kuzingatia kifungu cha 88 cha Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ya mwaka 2003 kinakataza kutengeneza, kuuza au kusambaza vipodozi vyenye sumu au athari kwa watumiaji”
Mkaguzi huyo ameongeza kuwa sheria hiyo inatoa tamkokwa baadhi ya viambata ambavyo haviruhusiwi kutumika katika vipodozi vyote na hii ni kutokana na athari zinazoweza kutokea
kutokana na matumizi yake.
Viambato hivyo ni pamoja na Bithionol, Hexachlorophene, Mercury compounds, Vinylchloride, Zirconium, Halogenated, Salicylanilides, Chloroquinone, Steroids, Chloroform, Chlofluorocarbon propellants na Methyelene chloride.
Kutokana na hali hiyo mwandishi wa gazeti hili amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi Mkoani Iringa wakaeleza kuwa mara nyingi vipodizo viliyokatazwa vina faida nyingi hivyo zoezi la kudhibiti kuwa gumu.
Bwana Mwetu Paulo, muuzaji wa duka la vipodozi katika eneo la Miyomboni manispaa ya Iringa anasema kuwa “Vipodozi vyenye madhara katika mwili wa binadamu bado vinapatikana vingi madukani kwa sababu ya njia za panya.”
Aliwalaumu watu walipewa dhama na serikali kulinda mipaka kuwa ndiyo chanzo cha kupitisha vipodozi hivyo. “Uzembe uko mipakani maana huko ndiko madawa na vipodozi viliyopigwa marufuku vinaingilia.” alisistiza Paulo.
Mfanya biashara wa vipodozi mnjini Iringa ambae hakutaka jina lake kutajwa anasema biashara hiyo ni ngumu kuidhibiti kwa kuwa wateja wake bado ni wengi na ndiyo wanaleta msukumo kwa wafanyabishara kuzileta bidhaa hizo sokoni.
“Unajua tinashawishiwa na watumiaji, ndiyo maana na sisi hatuachi kuviuza maana tunatafuta fedha kwa ajili ya kujikimu ki maisha.” alisema bila kujali madhara yake kwa binadamu.
Tonga Elisha, anauza vipodozi maeneo ya Semtema Iringa. Anasema kwamba wauzaji wengi hupenda kuuza bidhaa hizo haramu na zenye madhara ndani ya maduka yao, nikutokana na tama zao za kutaka fedha nyingi kutokana na faida yake uwa kubwa.
Aliongeza kuwa wateja wengi ambao ni wanawake hupenda kutumia vipodozi hivyo kuwa wanataka kuwa weupe na warembo maradufu huku wakisahau madhara ambyo wanaweza kuyapata.
Bwana Tonga Elisha alimalizia kwa kusema vitendo vya rushwa mipakani kunasabaisha vipodozi kuendelea kusambazwa na kuuzwa madukani hivyo anashauri Taasisi ya Kudhibii na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) iache kufanya kazi kwa mazoea.
Bi Rachael Mding’i ni mtumiaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku. yeye ni mkazi wa Semtema, Manispaa ya Iringa anasema “Mimi natumia kipodozi kitakachonifanya niwe mrembo na nadhifu na wala sijali juu ya madhara yanayoweza kutokea kwani nina muda mrefu natumia na wala sujapata kuona tatizo lolote lililojitokeza katika mwili wangu.”
Bi. Magreth Fanuel mkazi wa maeneo ya Tumaini mjini iringa. yeye amekuwa akitumia vipodozi kwa muda mrefu sasa. Alianza kutumia vipodozi kutokana na ushauri wa marafiki japo hana ufahamu wowote kuhusu vipodozi vyenye sumu.
“Ndugu mwandishi mimi nakiri kwamba sina elimu yoyote ya kivibaini vipodozi nyenye viambata vya sumu hivyo inakuwa vigumu kwangu kujua ni vipodozi gani vimepigwa marufuku.”
Hivyo ameishauri serikali kutoa elimu zaidi hata kwa njia mbalimbali ili watu wafahamu ni aina gani hasa pia wajue na madhara yake.
Mkaguzi huyo amebainisha adhabu ambazo zitachukuliwa kwa yeyote atakae kiuka sheria hizo katika kutengeneza, kusambazwa na kuuzwa kwa bidhaa haramu za vipodozi kuwa atatoa faini au kifungo pia atatozwa gharama za uteketezwaji wa hizo bidhaa alizokutwa nazo.
Mwisho anatoa wito kwa wauzaji na watengenezaji wote wafuate sheria walizopewa katika kufanya biashara zao pia kwa wanainchi kuacha kutumia bidhaa hizo ili kujiepusha na madhara kwa baadae kama kupata kansa, miwasho, vipele, kuchubuka na saratani kama ya damu, ubongo, figo na mapafu.
No comments:
Post a Comment