Ndugu Joseph Malongo, Mtangaza nia wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi |
Nzega.
Aliyekuwa mgombea
wa ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini kwa
tiketi ya Chadema , Joseph Malongo
ametangazi nia ya kugombe nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi
katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu.
Kijana huyo
machachari ameyasema maneno hayo leo alipokuwa
akizungumza na mwandishi wetu, na kuelezea kwamba amefikia uamuzi huo ii
kukiwezesha chama chake kusimama imara katika kanda ya Magharibi hasa wakati
huu ambao taifa linakabiliwa na ukandamizwaji wa demokrasia.
Ameongeza kuwa “Safari
ya mabadiliko ndiyo imeanza, na Jumatatu natarajia kuchua fomu ya kugombea
nafasi muhimu katika chama changu, shabha yangu kubwa ni kutetea misingi ya
demokrasia ambayo imekuwa ikiminywa kila kukicha.”
Malongo ambaye
alionyesha upinzani mkubwa kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr
Hamis Kigwangala katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 amesema vijana ndani ya
chama wanayo nafasi kubwa kujitokeza katika kukijenga chama ili kiwafikie
wananchi.
“Ni wakati sasa
nataka nikitumikie chama changu kwa nguvu mpya na kukiimairisha ikiwa ni
maamndalizi ya kushika dora hapo mwaka 2020” alisema Malongo.
Diwani huyo wa zamani
wa kata ya Nata ameeleza kuwa wanachi wengi wamechoshwa na serikali ya CCM, hivyo wanatafuta chama mbadala
ili kuwaletea mabadiliko ya kweli, “kama mwanachadema nina haki ya demokrasia
hivyo nitagombea ili kukiimashisha chama changu.
Mlongo a,bye ni
Msomi wa wa Shahahada ya Utwala katika Biashara aliongeza kuwa ni atatumia
elimu yake kuweka misingi ya kuinua
uchumi wa chama ili kiweze kujitegemea ili kiweze kuwafikia wananchi wengi
vijijini.
Ili tuishinde CCM
2020 tunahitaji wapiga kura, na wakati wa kuvuna wapiga kura ni sasa… nawaomba
wana Chadema wenzangu kanda ya Magharibi waniunge mkono tufanye kazi kwa pamoja
kuking’oa madarakani chama chakavu.
No comments:
Post a Comment