Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Profesa. Nicholas Bangu anawaalika wahitimu wa mwaka 2011, familia, ndugu, jamaa, marafiki na umma kwa ujumla kwenye mahafali ya 14 ya chuo hicho yatakayofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Oktoba mwaka huu. Mahafali yataanza saa 3:00 asubuhi chuoni hapo.
Mahafali yatatanguliwa na kongamano la wanataaluma (convocation) litakalofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Oktoba, kuanzia saa 3:30 asubuhi chuoni hapo.
Wahitimu wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao na kuhudhuria mazoezi ya mahafali (rehearsal) bila kukosa. Wanafunzi wasiyohudhuria mazoezi hayo yatakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Oktoba, saa 10:00 Jioni hawatashiriki kwenye mahafali.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kutuma ujumbe (SMS) kwa simu namba 0767888596 ama barua pepe (email) pro@tumaini.ac.tz. Mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni tarehe 23/10/2011.
Majoho ya mahafali yataanza kutolewa tarehe 24/10/2011. Mwisho wa kutoa mahojo ni tarehe 28 Oktoba 2011 saa 10:00 jioni. Majoho yatatolewa na ofisi za wakuu wa vitivo husika.
NYOTE MNAKARIBISHWA
No comments:
Post a Comment