Wednesday, June 28, 2017

TFDA Yatangaza Vita Wauza Vipodozi Feki Mkoani Iringa

Baadhi ya vipodozi vya aina mbalimbali vikiwa katika moja ya maduka mkoani Iringa tayari kwa watumiaji kuja kuvinunua. (Picha na Sabinus Paulo)

John Masanja,
Mwandishi Iringa Kwetu

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Nyanda za Juu Kusini imetoa tahadhali kwa watu wanaoendelea kutumiwa vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani ni hatari kwa faya zao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mamlaka ili kudhibiti bidhaa hizo.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa gazeti la Iringa Kwetu Mkaguzi wa Dawa, TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dk Sylvester Mwidunda amesema kuwa mamlaka hiyo imebaini kuwa bado suala la utengenezaji, usambazaji na uuzaji wa vipodozi
vyenye sumu unaendelea.

Mwidunda amesema “Kwa kuzingatia kifungu cha 88 cha Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ya mwaka 2003 kinakataza kutengeneza, kuuza au kusambaza vipodozi vyenye sumu au athari kwa watumiaji”

Mkaguzi huyo ameongeza kuwa sheria hiyo inatoa tamkokwa baadhi ya viambata ambavyo haviruhusiwi kutumika katika vipodozi vyote na hii ni kutokana na athari zinazoweza kutokea
kutokana na matumizi yake.

Viambato hivyo ni pamoja na Bithionol, Hexachlorophene, Mercury compounds, Vinylchloride, Zirconium, Halogenated, Salicylanilides, Chloroquinone, Steroids, Chloroform, Chlofluorocarbon propellants na Methyelene chloride.

Kutokana na hali hiyo mwandishi wa gazeti hili amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi Mkoani Iringa wakaeleza kuwa mara nyingi vipodizo viliyokatazwa vina faida nyingi hivyo zoezi la kudhibiti kuwa gumu.

Bwana Mwetu Paulo, muuzaji wa duka la vipodozi katika eneo la Miyomboni manispaa ya Iringa anasema kuwa “Vipodozi vyenye madhara katika mwili wa binadamu bado vinapatikana vingi madukani kwa sababu ya njia za panya.”

Aliwalaumu watu walipewa dhama na serikali kulinda mipaka kuwa ndiyo chanzo cha kupitisha vipodozi hivyo. “Uzembe uko mipakani maana huko ndiko madawa na vipodozi viliyopigwa marufuku vinaingilia.” alisistiza Paulo.

Mfanya biashara wa vipodozi mnjini Iringa ambae hakutaka jina lake kutajwa anasema biashara hiyo ni ngumu kuidhibiti kwa kuwa wateja wake bado ni wengi na ndiyo wanaleta msukumo kwa wafanyabishara kuzileta bidhaa hizo sokoni.

“Unajua tinashawishiwa na watumiaji, ndiyo maana na sisi hatuachi kuviuza maana tunatafuta fedha kwa ajili ya kujikimu ki maisha.” alisema bila kujali madhara yake kwa binadamu.

Tonga Elisha, anauza vipodozi maeneo ya Semtema Iringa. Anasema kwamba wauzaji wengi hupenda kuuza bidhaa hizo haramu na zenye madhara ndani ya maduka yao, nikutokana na tama zao za kutaka fedha nyingi kutokana na faida yake uwa kubwa.

Aliongeza kuwa wateja wengi ambao ni wanawake hupenda kutumia vipodozi hivyo kuwa wanataka kuwa weupe na warembo maradufu huku wakisahau madhara ambyo wanaweza kuyapata.
Bwana Tonga Elisha alimalizia kwa kusema vitendo vya rushwa mipakani kunasabaisha vipodozi kuendelea kusambazwa na kuuzwa madukani hivyo anashauri Taasisi ya Kudhibii na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) iache kufanya kazi kwa mazoea.

Bi Rachael Mding’i ni mtumiaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku. yeye ni mkazi wa Semtema, Manispaa ya Iringa anasema “Mimi natumia kipodozi kitakachonifanya niwe mrembo na nadhifu na wala sijali juu ya madhara yanayoweza kutokea kwani nina muda mrefu natumia na wala sujapata kuona tatizo lolote lililojitokeza katika mwili wangu.”

Bi. Magreth Fanuel mkazi wa maeneo ya Tumaini mjini iringa. yeye amekuwa akitumia vipodozi kwa muda mrefu sasa. Alianza kutumia vipodozi kutokana na ushauri wa marafiki japo hana ufahamu wowote kuhusu vipodozi vyenye sumu.

“Ndugu mwandishi mimi nakiri kwamba sina elimu yoyote ya kivibaini vipodozi nyenye viambata vya sumu hivyo inakuwa vigumu kwangu kujua ni vipodozi gani vimepigwa marufuku.”

Hivyo ameishauri serikali kutoa elimu zaidi hata kwa njia mbalimbali ili watu wafahamu ni aina gani hasa pia wajue na madhara yake.

Mkaguzi huyo amebainisha adhabu ambazo zitachukuliwa kwa yeyote atakae kiuka sheria hizo katika kutengeneza, kusambazwa na kuuzwa kwa bidhaa haramu za vipodozi kuwa atatoa faini au kifungo pia atatozwa gharama za uteketezwaji wa hizo bidhaa alizokutwa nazo.

Mwisho anatoa wito kwa wauzaji na watengenezaji wote wafuate sheria walizopewa katika kufanya biashara zao pia kwa wanainchi kuacha kutumia bidhaa hizo ili kujiepusha na madhara kwa baadae kama kupata kansa, miwasho, vipele, kuchubuka na saratani kama ya damu, ubongo, figo na mapafu.

Mpango wa Elimu Bure Waibua Mapya Iringa

Baadhi ya wanafunzi wa Secondary mkoani Iringa wamemebeba komputer kuelekea darasa maalumu kwa ajili ya kujifunza. Tanzngu mpango wa Elimu Bure uanzwe kutekelezwa mkoani hapa zipo chngamoto kadha wa kadha zimeanza kujitokeza.


Na Mwanaidi Waziri, Joan Victor

Waandishi-Iringa Kwetu

Utekelezaji wa mpango wa elimu bure uliotolewa na Rais John Magufuli umeibua changamoto kadhaa licha ya kuwa na faida nyingi ikiwamo ongezeko la wanafunzi mashuleni na kupunguza mzigo kwa wazazi masikini nchini.

Haya yamebainika kufuatia wazazi wengi kutoonesha ushirikiano wowote katika masuala ya kielimu
yanayowahusu watoto wao kwa kile wanachodai serikali ndio inashughulikia masuala yote ya elimu hivi sasa kutokana na tamko lake la elimu bure.

Aidha imeonekana kuwa walimu wamekuwa wavivu na kutokuwa makini mashuleni tangu kuanzishwa kwa mpango huo jambo ambalo wazazi wengi wamelilalamikia na kuiomba serikli kushughulikia hali hii kwani inaathiri maendeleo ya watoto kielimu.

Akizungumza na Iringa Kwetu hivi karibuni, Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Ndugu William Mafwele, amesema suala zima la elimu bure lina faida na changamoto zake kutokana na vile baadhi ya watu walivyolipokea na kulitafsiri katika jamii.

Mkurugenzi ameelezea mchakato mzima wa mpango huo ulivyoanza akisema: “Tulilipokea vizuri tamko la Mhe. Rais na mchakato wa utekelezaji wake ulienda vizuri kwa kiwango cha wanafunzi kuongezeka kwa asilimia 68 na ufaulu pia unaongezeka kufuatia watoto wengi kuhudhuria mashuleni bila kubughudhiwa ada ya aina yeyote.”

Kwa upande mwingine, ameongelea changamoto mbali mbali ambazo zinatokana na mpango huu wa elimu bure ikiwemo wazazi kubweteka na kutokutaka kushiriki chochote katika masuala ya maendeleo ya elimu kwa vile serikali imesema “elimu bure”.

Muhadhili wa Chuo Kikuu cha Iringa na mtaalamu wa mambo ya elimu, Dk. Lucas Mwaombela amesema wazo la serikali kuanzisha mpango wa elimu bure ni jema kwani limelenga kuhakikisha kila mtanzania mwenye umri wa kwenda shule anapata elimu bila kikwazo.

Ingawa mpango huu umeonesha kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili “elimu bure”, Dk Mwaombela anasema “Kila mpango mzuri unazalisha changamoto” na kuongeza kuwa kuwa serikali umeonyesha juhudi kubwa katika kukabiliana na changamoto hizo.

Wito wangu kwa serikali na wadau wote wa elimu nchini, jambo la elimu sio suala la serikali peke yake, tunapaswa kujitoa kuchangia elimu lakini pia serikali itoe ajira za walimu maana tuna walimu wa kutosha wapo mtaani wakisubiri ajira.

Kaimu Afisa wa Elimu Manispaa ya Iringa mjini ambaye hakutaka jina lake litajwe aliongeza kuwa suala la elimu bure limesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi kitu ambacho kimepelekea walimu
kupunguza mitihani mashuleni kuepuka kazi nyingi suala ambalo linapunguza umakini wa wanafunzi katika masomo.

Gazeti la Iringa Kwetu limeshuhudia baadhi ya wazazi wakilalamikia mpango huo kwa kile wanachodai umepunguza umakini wa walimu mashuleni ukilinganisha na hapo awali suala ambalo serikali hailiangalii kwa umakini.

Beti Chengula, ambaye ni mfanya biashara katika soko kuu la manispaa ya Iringa ameliambia gazeti hili kuwa mpango wa elimu bure si mzuri kwasababu walimu hawafanyi kazi kwa bidii tangu uanzishwe na hawapo makini katika ufundishaji wala usimamizi wa watoto mashuleni.

Ameongeza kuwa tangu serikali ianzishe mpango huu, maendeleo ya mtoto wake si mazuri ukilinganisha na hapo awali yalivyokuwa na ndio sababu yeye haoni faida ya elimu kuwa bure na kutoa rai kwa walimu kufundisha kwa moyo kama inavyotakiwa kwa kuwachukulia wanafunzi
kama watoto wao.

Licha ya changamoto mbalimbali zinazotokana na mpango huu wa elimu bure wa serikali, Iringa
Kwetu imeshuhudia baadhi wa wazazi wakiipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua iliyoifikia ya kuifanya.

Sumatra:Wanaopandisha Nauli Sikukuu Kukiona

Baadhi ya mabasi yakisubiria abiria katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Iringa. Imekuwa ni desturi kwa wamiliki wa mabasi kupandisha nauli wakati wa msimu wa skukuu za Krismas na Mwaka Mpya (Picha Na Sabinus Paulo).

Na Stephan Ngolongolo
Mwandishi- Iringa Kwetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imetoa onyo kali kwa wasafirishaji kutokupandisha nauli kulelekea msimu wa sikukukuu za Krismas na Mwaka mpya.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni, Afisa Mfawidhi SUMATRA Mkoa wa Iringa, Ngereza Pateli amesema kuwa kitendo cha kupandisha nauli bila idhini ya mamalaka hiyo ni kinyume na sheria ya usafirishaji.

Aidha afisa huyo amewataka wananchi kutumia namba 15276 ili kupata taarifa zinazohusiana na viwango vya nauli na bei elekezi, huduma ambayo hutolewa na mamlaka hiyo. Ili kupata taarifa, abiria anatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maandaishi kupitia simu yake ya mkononi kwa kuandika neno nauli, anaacha nafasi, kisha anaandika mahali anapotaka kusafiri kisha anachagua daraja la basi husika na kuutuma ujumbe huo kwenda namba tajwa hapo huu.

“Kupandisha nauli bila idhini ya mamlaka ni kosa kisheria... kwa hiyo nitoe wito kwa wamiliki wa wote mabasi wasifanye hivyo, kwani tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria.” Alisema Pateli.

Afisa huyo aliongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kupandisha bei ya nauli hususani kwa mabasi yanayofanya safari za mikoani wakati wa msimu wa sikukuu. Kwa upande wake, Wakala wa Mabsi ya Delux, Julius Eziudy amesema tatizo la kupandisha bei za nauli wakati wa sikuku limekuwa sugu mkoni Iringa linalosabaishwa na wapiga debe.

Alikiri kuwa mara nyingi msimu wa sikukuu ipo changamoto kubwa ya uhaba wa magari ingawa kwa upande wa kampuni yao wana magari ya kutosha hivyo kuwatoa hofu wateje wao na kuwataka
wafike mapema kukata tiketi. 

“Kama ikitokea magari yetu yote yamejaa huwa tuanomba vibali vya muda mfupi na kutumia magari wa watu wengine kutoa huduma kwa wateja wetu.” Alisisitiza. 

Mwenyekiti wa Umoja waWakatishaji Tiketi stendi kuu ya mabasi mkoani Iringa, Erasto Gasper amesema uzoefu unaonesha baadhi ya abiria wanatambua utaratibu wa kukata tiketi tofauti na hapo nyuma.

Mtalemwa Alex ni kondakta wa mabasi ya Kampuni ya Mwendamseke. Anasema kuwa msimu kama huo ukifika wanapata faida kubwa kutokana na kuwepo kwa abiria wengi hivyo wapiga debe wanalazimika kupandisha nauli bila utaratibu.

Kwa mujibu wa Pateli, SUMATRA kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafirishaji kama, polisi wa usalama barabarani wamejipanga kuhakikisha kwamba hakuna adha ya usafiri kuelekea Krismas na mwaka mpya.

“Tumelitambua jambo hilo, hivyo tumejipanga kufanya ukaguzi wa magari kuanzia asubuhi
mpaka jioni.” Aliongeza “Pia tumekuwa tukitoa elimu kupitia vyombo vya habari kuwataka wananchi wakate tiketi kwenye ofisi huska ili kuepusha ulaghai.”

x

Taifa Stars yatoa Sare tasa na Botswana





Timu ta Taifa ya Tanzania (Taifa stars) leo imetoa sare ya kutokufunga na Timu ya Angola katika michuano ya COSAFA 2017 inayoendelea nchini Africa ya Kusini.

Game za leo Tanzania ilicheza dhidi ya Angola na kulazimishwa sare tasa wakati game ya Malawi na Mauritius imemalizika kwa sare tasa pia hivyo Tanzania bado anaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli, michuano hii ya COSAFA 2017 timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.