Friday, August 12, 2016

Mpinzani wa Kigwangala kujitosa Uenyekiti wa Kanda-Chadema

Ndugu Joseph Malongo, Mtangaza nia wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema  Kanda ya Magharibi



Nzega.  

Aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini  kwa tiketi ya Chadema , Joseph  Malongo ametangazi nia ya kugombe nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu.

Kijana huyo machachari ameyasema maneno hayo  leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu, na kuelezea kwamba amefikia uamuzi huo ii kukiwezesha chama chake kusimama imara katika kanda ya Magharibi hasa wakati huu ambao taifa linakabiliwa na ukandamizwaji wa demokrasia.

Ameongeza kuwa “Safari ya mabadiliko ndiyo imeanza, na Jumatatu natarajia kuchua fomu ya kugombea nafasi muhimu katika chama changu, shabha yangu kubwa ni kutetea misingi ya demokrasia ambayo imekuwa ikiminywa kila kukicha.”

Malongo ambaye alionyesha upinzani mkubwa kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr Hamis Kigwangala katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 amesema vijana ndani ya chama wanayo nafasi kubwa kujitokeza katika kukijenga chama ili kiwafikie wananchi.
“Ni wakati sasa nataka nikitumikie chama changu kwa nguvu mpya na kukiimairisha ikiwa ni maamndalizi ya kushika dora hapo mwaka 2020” alisema Malongo.

Diwani huyo wa zamani wa kata ya Nata ameeleza kuwa wanachi wengi wamechoshwa na  serikali ya CCM, hivyo wanatafuta chama mbadala ili kuwaletea mabadiliko ya kweli, “kama mwanachadema nina haki ya demokrasia hivyo nitagombea ili kukiimashisha chama changu.

Mlongo a,bye ni Msomi wa wa Shahahada ya Utwala katika Biashara aliongeza kuwa ni atatumia elimu yake  kuweka misingi ya kuinua uchumi wa chama ili kiweze kujitegemea ili kiweze kuwafikia wananchi wengi vijijini.


Ili tuishinde CCM 2020 tunahitaji wapiga kura, na wakati wa kuvuna wapiga kura ni sasa… nawaomba wana Chadema wenzangu kanda ya Magharibi waniunge mkono tufanye kazi kwa pamoja kuking’oa madarakani chama chakavu.